Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United ya Uingereza Sir Alex Ferguson ameshangazwa na uamuzi wa klabu ya Juventus ya Italia kusuasua kufanya maamuzi ya kumuuza kiungo Paul Pogba katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania.
Ferguson anaamini ingekuwa busara zaidi kama Klabu ya Juventus ingemuuza kiungo huyo katika klabu ya FC Barcelona ambao wameonesha dhamira ya dhati ya kumuhitaji nyota huyo raia wa kifaransa.
Ferguson anawashangaa Juventus kujishauri kumuuza nyota huyo kwa dau linalokadiriwa kufikia zaidi ya pound milion 50 licha ya yeye kumuacha ajiunge na Juventus kama mchezaji huru mwaka 2012.
Watendaji wa FC Barcelona na watendaji wa Juventus walikutana wiki iliyopita na kukubali kutoa kiasi cha zaidi ya pound milioni 50 kama ada ya uhamisho wa Pogba ambacho Ferguson anaamini walifanya makosa kukataa offer hiyo.
“Ningemuuza Pogba, kama ningekuwa Juve leo hii ningemuacha aende” >>> Ferguson.
Hata hivyo Ferguson aliwapongeza Juventus kwa kutwaa taji la Serie A msimu uliopita na kufika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya licha ya kufungwa na FC Barcelona.
“Juve wana
timu bora, wamewahi kutwaa taji la Serie A mara nne mfululizo, kwa
mtazamo wangu walikuwa hawana bahati katika mchezo wa fainali ya klabu
bingwa Ulaya, walifungwa na Barcelona kwa mashambulizi ya kushtukiza
kabla ya hapo waliutawala mchezo” >>> Ferguson.
No comments:
Post a Comment