Wabunge Ukawa wakimbilia CCM
More information about text formats
ANGALAU wabunge wanne kutoka katika vyama vinavyounda
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) watahamia Chama
Cha Mapinduzi (CCM) mara baada ya kuvunjwa kwa Bunge
hili la 10, Raia Mwema limeambiwa.
Wabunge hao wamedaiwa kuanza mipango hii na gazeti hili
linafahamu kuwa wabunge hao wanne tayari
wamezungumza na CCM wiki hii na wakati wowote baada ya
kuvunjwa kwa Bunge wanaweza kutangazwa.
Gazeti hili limeambiwa na vyanzo vyake vya kuaminika
kwamba mojawapo ya sababu ya wabunge hao kurejea CCM
ni kutaka watumie fedha zao za mafao ya kustaafu pasipo
kuchangia vyama vyao kama ilivyo utaratibu kwenye baadhi
ya vyama vya upinzani nchini.
Kwa mujibu wa Kamati ya Huduma za Bunge, wabunge wa
Bunge la 10 watalipwa kiinua mgongo chao chenye thamani
ya shilingi milioni 230 kila mmoja; na wapo wabunge ambao
hawataki ‘ kugawana na vyama vyao’ fedha hizo.
“ Kwenye vyama vya upinzani kuna utaratibu wa wabunge
kuchangia vyama vyao. Vyama kama CUF kwa mfano,
wabunge wanakatwa kwenye mishahara yao kila mwezi kwa
ajili ya kusaidia shughuli za chama chao.
“Ruzuku peke yake haitoshi na ndiyo maana mojawapo ya
vyanzo vya mapato vya vyama vya siasa ni michango kutoka
kwa wabunge wao. Sasa kuna hofu kuwa wapo wabunge
ambao safari hii hawatapitishwa kwa sababu ya makubaliano
ya Ukawa kugawana majimbo.
“ Mtu anaona bora ahamie zake CCM na achukue kiinua
mgongo chake mapema maana akibaki kwenye chama chake
atakatwa na ubunge hatapata. Hawa wanne najua watakuja,”
kilisema chanzo chetu cha kuaminika ambacho ni mojawapo
ya viongozi wa kitaifa wa CCM.
Raia Mwema limeambiwa kwamba vyama ambavyo
vitaathirika na hatua hii ni CUF na Chadema ambavyo ndivyo
vyenye wabunge wengi kuliko NCCR Mageuzi na NLD
ambayo haina mbunge hata mmoja hadi sasa.
Akizungumzia madai hayo, Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe, alisema chama chake hakijatoa agizo lolote
la kutaka wabunge wake wachangie fedha kutokana na
malipo ya mafao ya kiinua mgongo.
“Sisi kama Chadema hatujawahi kumlazimisha mbunge wetu
achangie chama kwa nguvu. Suala hili limekuwa la
maridhiano na wakati mwingine imekuwa kawaida kwa
wabunge kukikopesha chama na baadaye wakalipwa.
“ Sidhani kama kuna mbunge wa Chadema anaweza kuhama
chama chake kwa sababu hiyo. Kama ni kwa sababu nyingine
labda lakini hiyo sidhani. Nakuhakikishia kwamba hakuna
mbunge yeyote aliyelazimishwa kuchangia,” alisema Mbowe.
Juhudi za kumpata Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Profesa
Ibrahim Lipumba, kuzungumzia suala hilo hazikufanikiwa
hadi wakati tunakwenda mitamboni.
Raia Mwema linazungumza na wabunge hao wanne wa
Ukawa wanaodaiwa kutaka kujiunga na CCM na yakikamilika
majina yao yatawekwa hadharani.
Sunday, July 12, 2015
Wabunge wa ukawa kuhamia ccm.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment