Vazi la Burqa lapigwa marufuku Cameroon
Maafisa
wa serikali kaskazini mwa Cameroon wamepiga marufuku wanawake kuvalia
vitambara vinavyofunika nyuso zao maarufu kama Burka.
Uamuzi huo
umechukuliwa kufuatia mashambulio ya mabomu yaliyotekelezwa na wanawake
waliokuwa wamevalia Burka, wanaoaminika kuwa wafuasi wa kuni la Boko
Haram.Gavana wa jimbo la Far, amesema kuwa raia katika eneo hilo hawataruhusiwa kuendesha magari yenye vioo vilivyotundikwa karatasi maalum inayozuia watu kuona ndani.
Aidha uendeshaji wa piki piki umepigwa marufuku nyakati za usiku.
Siku ya Jumatano Gabon ilipiga marufuku wanawake kuvalia Burka hadharani na kazini kwa sababu ya mashambulio hayo yaliyofanyika nchini Cameroon.
Mwezi uliopita Chad pia ilipiga marufuku wanawake kuvalia Burka.
No comments:
Post a Comment