ATM ya Maji yazinduliwa Kenya
- 12 Julai 2015
Wakazi
wa kitongoji duni cha Mathare katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, sasa
wanaweza kupata maji safi ya kunywa na kwa matumizi mengine.
Mpango
unaoungwa mkono na serikali umezinduliwa kwenye mji mkuu wa Kenya
Nairobi unaowawezesha watu wanaoishi kwenye mitaa ya mabanda kununua
maji kwa kutumia kadi.Vituo vya kuuza maji vimebuniwa kote katika sehemu za mabanda ambapo wenyeji hutumia kadi zilizo na pesa kununua maji safi na kwa bei nafuu.
Mradi kama huo umefaulu katika baadhi ya maeneo ya vijijini nchini Kenya, lakini hii ni mara ya kwanza kuzinduliwa katika mji huo mkuu.
Kampuni ya kusimamia huduma ya usambazaji maji, ina mikakati ya kuhakikisha kuwa huduma hii walioianzisha itasambazwa kote katika mji mkuu wa Nairobi na kwengineko nchini humo.
No comments:
Post a Comment