Mbio za kuelekea uchaguzi mkuu katika
klabu ya Fc Barcelona bado zinaendelea na wagombea wanne kati ya saba
wametimiza vigezo vya kuendelea hatua inayofuata ya kuwania fursa ya
kuwa raisi wa klabu hiyo kwa miaka sita.
Miongoni mwa vigezo wa kuendelea na
hatua inayofuata katika mbio hizo za uraisi ni lazima mgombea apate
saini za mashabiki wa klabu hiyo kuanzia 2534 na kuendelea.
Wamebakia wagombea wanne waliofuzu
kigezo hicho na watatu kuenguliwa. Walioabakia katika mbio hizo za
kuwania nafasi ya uraisi ni raisi wa sasa Josep Maria Bartomeu, Joan
Laporta, Augusti Benedito na na msemaji wazamani wa klabu hiyo Toni
Freixa Here. Wafuatao ni wagombea wanne wa uraisi waliofuzu katika
mchujo wa kwanza na mipango yao kwa klabu hiyo.
- Josep Maria Bartomeu (52) ndiye raisi wa sasa wa klabu hiyo na aliingia madarakani kuchukua nafasi ya Sandro Rosell January 2014 ambaye alijiuzulu kutokana na tuhuma ya usajili wa Naymer.
- Joan Laporta (53) huyu aliwahi kuwa raisi wa klabu hiyo kuanzia mwaka 2003-2010 anafahamika kwa kusajili mastar klabuni hapo ndiye aliewaleta Ronaldinho,Eto’o na makocha kama Frank Rijkard na Pep Guardiola klabuni hapo.
Laporta ahadi yake kubwa klabuni hapo
kama atachaguliwa kuwa raisi kwa awamu ya pili, atahakikisha Paul Pogba
anatua Camp Nou, atarejesha furaha ya nyota wao Lionel Messi ambaye siku
kadhaa nyuma iliripotiwa kuwa hana furaha klabuni hapo. Lakini pia
atarudisha ufalme wa kituo cha kukuzia wachezaji chipukizi wa klabu hiyo
La Masia na atamleta Eric Abidal kuwa mkurugenzi wa michezo klabuni
hapo.
- Augusti Benedito (51) ni mfanyabiashara wa kikatalunya ambaye pia anatajwa kuwa miongoni mwa watu waliokuwa wanampinga raisi wa zamani wa klabu hiyo Josep Lluis Nunez mwaka 1997. Benedito aliwahi kufanya kazi kazi klabuni hapo mwaka 2003 chini ya raisi Joan Laporta ,alijiuzulu mwaka 2009 kutokana na tofautika kati yake bodi ya klabu hiyo.
Benedito pia aliwahi kugombea uraisi wa
klabu hiyo mwaka 2010 na kushika nafasi ya pili baada ya Sandro Rosell
kushinda kwa asilimia 60.
Anacho kiamini ni kuwa mkataba na Qatar
una haribu sura ya klabu hiyo na akichaguliwa kuwa raisi atarudisha
Unicef mbele ya jezi ya timu hiyo licha ya kuwa Qatar wanalipia.
Miongoni mwa ahadi zake akiwa klabuni hapo ni kuwa kiungo wa Paris
Saint Germain (PSG) Marco Verratti yupo katika kiwango cha juu na endapo
ataingia madarakani atamleka Camp Nou. Atawarudisha klabuni hapo Pep
Guardiola na Jojan Cruyff yeye pia kama Laporta atarejesha heshima ya
kituo cha La Masia.
- Toni Freixa (47) alikuwa msemaji wa klabu hiyo katika utawala wa Sandro Rossel na Josep Bartomeu kati ya 2010-2014. Toni anapanga kuifanya Barcelona kuwa brand inayo ongoza duniani na kuimarisha ubora wa La Masia na kusajili wachezaji bora kutoka kila kona ya dunia.
Fc Barcelona inatarajia kufanya uchaguzi mkuu july 18 mwaka huu wa kuchagua raisi wa klabu hiyo, hata hivyo uchaguzi huo umepelekea kuchelewesha mipango mingi kusimama ikiwemo uhamisho wa Pedro Rodriguez kwenda Chelsea.
No comments:
Post a Comment