Stori kubwa mbili kutoka ITV >>> CUF kutoshiriki Kikao cha UKAWA, Mzee Kingunge kuhusu Mgombea wa CCM na LOWASSA..
Jana kulikuwa na Kikao cha Umoja wa
Vyama vya UKAWA, lakini katika Kikao hicho hakukuwa na Kiongozi yoyote
wa CUF, mitandaoni kukaanza kutembea uvumi kuhusu kutokuwepo kwao.
Nilikutana na #Tweets
kwenye ukurasa wa Gazeti la MWANANCHI ambazo walikuwa wamemnukuu
Kiongozi wa CUF Magdalena Sakaya kuhusu sababu za CUF kutokuwepo.
Stori imeingia kwenye Headlines tena kwenye habari ya ITV kuhusu ishu hiyo, July 11 2015 Professa Lipumba alisema kwamba CUF watamtangaza mgombea wao July 14 2015 lakini haikuwa hivyo.
>>>> “Professa
Lipumba alisema hivyo baada ya kujua kwamba tutakaa na Viongozi wengine
tufikie maamuzi lakini ikatokea tofauti kabisa… Sisi ndani ya CUF
hakuna Kiongozi yoyote mwenye mamlaka ya kuamua tatizo gumu ambalo
linatakiwa kuamriwa na Kikao husika, hata mimi naweza kufukuzwa muda
wowote kama nikikiuka taratibu kama hizo…“>>>> Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu CUF Tanzania Bara.
Kwenye Kikao cha Viongozi wengine wa
UKAWA waliokutana jana walisema tayari wamempata Kiongozi wa kuwakilisha
UKAWA japo CUF hawakushiriki Mkutano huo >>> “Kwa
mashauri tuliyoyafanya, tumefanikiwa kwa njia ya maridhiano kumpata
Mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya UKAWA kwenye Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba 2015…” >>>> James Mbatia.
MZEE KINGUNGE KUHUSU MCHAKATO WA KUMPATA MGOMBEA URAIS CCM.
Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru amekuwa
mmoja ya Wanachama wa CCM ambao wamejitokeza kupinga utaratibu
uliotumika kumpata Mgombea wa CCM siku chache baada ya Chama hicho
kumtangaza Mgombea wa Urais wao kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
>>> “Kitendo
cha kuinyang’anya Kamati Kuu kazi yake sio cha kawaida, ni uvunjifu wa
taratibu na hakuna uadilifu ndani yake… Kamati ya Maadili yenyewe
inavunja maadili, maadili ya Chama yananzia kwenye kuheshimu muundo wa
Chama na taratibu zake” >>>> Mzee Kingunge.
Mzee Kingunge anapinga pia kuhusu utaratibu uliotumika kumpata Mgombea wa Urais >>>> “Kamati
Kuu inapelekewa orodha ya watu watano wapitishwe, hawa Wagombea wote 38
waliorudisha fomu hawakuwaona, hawakupita mbele yao, hawakuwauliza
maswali na hata kwenye Kamati ya Maadili naamini hawakuitwa.. Kuna watu
wachache wamekaa wakatengeneza orodha yao” >>>> Mzee Kingunge.
Kingine ni hiki alichokisema kuhusu Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa >>>> “RICHMOND
imempa ushindi Lowassa, kwa sababu Serikali yenyewe imekiri hakuna
lililoharibika pale, yeye aliwajibika kisiasa.. ndani ya Bunge kulikuwa
na kundi kubwa nia yao ni kumchafua Edward kwa sababu zao Kisiasa.” >>>> Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru.
No comments:
Post a Comment