DMX kwenye headlines, ajikuta matatani baada ya hukumu hii kutolewa mahakamani!
Headlines kwenye kurasa za burudani siku ya leo zinaandikwa na rappa maarufu kutoka Marekani, DMX.
Mwanzoni kulikua na kesi inayomhusu DMX
kukwepa majukumu ya kumtumia aliyekuwa mke wake hela ya matunzo ya
mtoto wao, DMX akapewa onyo na kuambiwa awe analipa hela hiyo,
akakubali.
Kesi imerudi tena mahakamani, gharama za hela zote alizokuwa anakwepa kulipa matunzo ya mwanae sasa imefika dola 400,000 sawa na Mil. 800 za Kitanzania. Mahakama imetoa maamuzi na imesema jamaa atatumikia adhabu ya miezi sita jela kwenye Erie County Holding Center.
Licha ya hayo msanii huyu anashitakiwa kwa makosa mengine madogo, mwezi wa nne mwaka huu DMX na bodyguard wake walishitakiwa kwa kosa la kupora na kuiba kwa kutumia silaha ambako walimuibia mtu dola 3,200 sawa na Mil 6,400,000 za Kitanzania jijini New Jersey, kosa ambalo bado analikataa.
>>>“Sikumbuki
kama nilishawahi kufanya kitu kama hicho mwezi wa nne, ndio tulikuwa
New Jersey na nakumbuka tu kusimama Petrol Station na kuweka mafuta
kwenye gari langu, hicho kitu mimi sijawahi kufanya, na kwa nini
nifanye, shetani kila siku ananiandama ila I am special to God”. >>> DMX.
uko
No comments:
Post a Comment