KHAMENEI:Iran haitabadili sera
Kongozi
mkuu nchini Iran Ayatollah Khamenei amasema kuwa makubaliano kuhusu
mipango ya nyuklia yaliyoafikiwa na mataifa makubwa duniani wiki
iliyopiya hayawezi kubadili sera za Iran eneo la mashariki ya kati.
Akizungumza
kupitia kwa runinga ya taifa kuadhimisha kumalizika kwa mwezi mtukufu
wa Ramadhan, Ayatolla alisema kuwa Iran itaendelea kuwaunga mkono
washirika wake eneo hilo wakiwemo serikali ya rais Bashar al Assad
nchini syria, waasi wa Houthi nchini Yemen na wanamgambo wa Hamas katika
utawala wa Palestina.Amesema kuwa hakutakuwa na majadiliano yoyoye na marekani ambayo imekubali kuiondolea vikwazo vya kiuchumi ilivyoiwekea Iran ikilenga kufuatilia kwa makini mipango ya nyuklia ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment