Monday, February 15, 2016

Chui aliyevamia shule India atoweka

Chui aliyevamia shule India atoweka

  • Dakika 57 zilizopita
Chui aliyeingia kwenye shule India na kujeruhi watu sita ametoroka kutoka eneo ambamo amekuwa akizuiliwa kwa matibabu, maafisa wamesema.
Chui huyo wa umri wa miaka minane aliingia kwenye shule moja mjini Bangalore, Kundalahalli tarehe 8 Februari na kujeruhi watu hao kabla ya kutulizwa na kukamatwa.
ChuiImage copyrightPress Trust of India
Image captionChui huyo alijeruhi watu waliokuwa wakisadia kumkamata
Alipelekwa kwenye mbuga ya taifa ya wanyama ya Bannerghatta kwa matibabu na kuwekwa kwenye kizimba lakini akatoroka Jumapili.
Maafisa wanasema hakuna haja ya watu kuwa na wasiwasi.
"Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwani ingawa ametoroka kutoka kizimbani, bado yumo ndani ya mbuga,” mkurugenzi wa mbuga hiyo Santosh Kumar ameambia wanahabari.
"Lakini tulitaka kumzuilia kwa siku kadha zaidi kwani alikuwa akipokea matibabu,” ameambia hazeti la Hindustan Times.
chuiImage copyrightKashif Masood
Image captionShule 142 zilifungwa baada ya chui mwingine kuonekana
Maafisa hao wanasema chui huyo alitoroka baada ya wafanyakazi wa mbuga hiyo kufungua kizimba ili kumlisha, labda kutokana na mlango kutofungwa vyema.
Chui kadha wameonekana karibu ana mji wa Bangalore na kusababisha shule 142 kufungwa kama tahadhari.

No comments:

Post a Comment