Wednesday, February 17, 2016

Matumaini ya tiba ya saratani

Matumaini ya tiba ya saratani

  • roryamaendeleo
Image captionSeli za saratani
Utafiti uliofanywa na wanasayansi unasema kuwa tiba ya saratani inayotengezwa huenda ikatoa chanjo ya kudumu ya ugonjwa huo ili kuuzuia kurudi.
Utafiti huo uliowasilishwa katika mkutano wa muungano wa sayansi endelevu za Marekani mjini Washington umeonyesha matokeo yasio ya kawaida.
Mojawapo ya matokeo hayo yameonyesha kwamba tiba yenye seli zenye kinga kwa jina T Cells ,ina ufanisi wa zaidi ya asilimia 90 katika wagonjwa wanaougua sana saratani ya damu.
Hatahivyo Daktari Alan Worsely wa utafiti wa Saratani nchini Uingereza ameiambia BBC kwamba bado wanahitaji mbadala kukabiliana na magonjwa mengine ya saratani.
Image copyrightScience Photo Library
Image captionSeli za saratani
''Tumekuwa tukitumia teknolojia hii ya seli za kijenetiki zilizo na kinga.Kufikia sasa imeonyesha ufanisi katika saratani hii ya damu.Tuseme kwamba tiba ya satarani ya damu ina ufanisi na ni wagonjwa kidogo pekee ambapo teknolojia hii imeshindwa kufanya kazi.Changamoto kuu sasa ni kuonyesha ni vipi tutaweza kutumia kielelezo hiki kutibu saratani nyengine.Ni vipi tutaanza kushughlikia tiba ya saratani ya kwenye tishu,''.Alisema daktari Alan Worsley.

No comments:

Post a Comment