Wednesday, February 17, 2016

Ndege za Cuba kuruka tena Marekani

Ndege za Cuba kuruka tena Marekani

  • roryamaendeleo
Image captionmawaziri wa Cuba na Marekani wakishikana mkono baada ya makubaliano ya safari za anga
Marekani na Cuba zimetiliana tena saini makubaliano ya kurejesha tena safari za ndege za abiria baina ya nchi hizo mbili kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka hamsini iliyopita.
Utiwaji wa saini ya makubaliano hayo ulikuwa ni baina ya waziri wa usafiri wa Marekani , Anthony Foxx na mwenziwe kutoka Cuba Adel Izquierdo Rodriguez, mjini Havana makubaliano hayo yatashuhudia safari lufufu za kila uchao baina ya mataifa hayo yaliyokuwa mahasimu hapo awali.
Matarajio ya kuanza kwa safari hizo ni baada ya mwezi mmoja,ingawa mpaka sasa kisheria ni Marufuku kwa raia wa Marekani kuitembelea Cuba kama mtalii.
Ki diplomasia uhusiano wa nchi mbili hizo ilianza kurejea zaidi ya takribani mwaka mmoja uliopita .Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Havana ameelezea juu ya makubaliano hayo ya hivi karibuni kwamba yamekuja baada ya ikulu ya Marekani kutafakari uwezekano wa safari za kiserikari za rais wa Cuba nchini Marekani.

No comments:

Post a Comment