Wednesday, February 17, 2016

Pluijm agoma kumtaja Cannavaro first eleven

Pluijm agoma kumtaja Cannavaro first eleven

By: roryamaendeleo / Posted: Wednesday 17th February 2016
pluijmKocha Mkuu wa Yanga, Mdachi, Hans van Der Pluijm.
pluijm
Said Ally, Dar es Salaam
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mdachi, Hans van Der Pluijm, amegoma kuzungumzia nafasi ya beki na nahodha wa kikosi hicho, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ndani ya kikosi chake cha kwanza baada ya beki huyo kurejea akitokea katika kipindi cha majeruhi.

cannavaro-FILEminimizer.jpg

Nadir Haroub ‘Cannavaro’.



Pluijm alikuwa anamtumia Cannavaro katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo sambamba na Kelvin Yondani kabla ya kuumia ambapo nafasi yake ikachukuliwa na Mtogo, Vincent Bossou.

Akizungumza na Championi Jumatano, Pluijm alisema kuwa kwa sasa ni mapema kuanza kuzungumzia nafasi ya beki huyo baada ya kurejea akitokea majeruhi ambapo anampa muda wa kujiweka sawa kabla ya kumrejesha ndani ya kikosi hicho.

“Kwa sasa ni mapema kuanza kuzungumzia nafasi ya Cannavaro kwenye kikosi cha kwanza kwani kama unavyojua ndiyo kwanza amerejea kutoka nje alipokuwa akisumbuliwa na majeraha ya kisigino.

“Nitakachokifanya kwa sasa ni kumpa muda wa kujinoa zaidi na kujiweka sawa kwa ajili ya kurejesha makali yake kwani kama unavyojua hajacheza kwa kipindi kirefu, hivyo atafanya mazoezi hayo ya kujiweka sawa kabla ya baadaye kumrejesha,” alisema Pluijm.

No comments:

Post a Comment