Wednesday, February 24, 2016

Ethiopia kuchukua hatua kali dhidi ya Oromi

Image captionEthiopia kuchukua hatua kali dhidi ya Oromia
Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ameonya kuwa serikali yake itachukua hatua kali dhidi ya makundi ya jamii ya Oromia yanayoendesha kampeini ya kujitenga.
Runinga ya taifa inamnukuu bwana Hailemariam akisema kuwa ''watu wenye nia ya kuharibu'' wanaofadhiliwa na taifa jirani la Eritrea, wameanzisha kampeini ya kujitenga.
Waziri huyo anasema kuwa makundi hayo yameanza kuwavizia wanajeshi na kuharibu mali ya umma kwa kuteketeza kwa nia ya kuchochea raia wawaunge mkono.
''Raia hata hivyo wameshang'amua ukweli wa mambo ni kuwatenganisha na serikali na wamekataa,''
''Nia yao ni kuijumu na kisha kuipindua serikali''alisema Hailemariam.
"Serikali imeamua kuchukua hatua kali kwa mujibu wa sheria''.
Jumatatu hii kundi la kupigania haki za kibinadamu la Human Rights Watch lenye makao yake huko Marekani lilitoa ripoti mpya ikishutumu vikosi vya usalama nchini Ethiopia kwa kutekeleza zaidi ya miezi minne ya mauaji, ukatili na kukamatwa kwa mamia ya waandamanaji katika eneo la Oromia.
Image copyright
Image caption''Nia yao ni kuijumu na kisha kuipindua serikali''alisema Hailemariam.
Shirika la Human Rights Watch linasema vikosi hivyo, vimetumia nguvu kupita kiasi kuzima maandamano hayo yaliyoanza Novemba 2015, kupinga mipango ya kupanua mamlaka ya jiji kuu la Addis Ababa.
Serikali imekanusha ripoti hiyo.
HRW inasema kuwa vikosi vya usalama ikiwemo jeshi, inadaiwa kufanya misako mikali dhidi ya waandamanaji katika eneo la Oromia.
Oromia ndilo jimbo kubwa zaidi nchini Ethiopia.

Maandamano hayo yalianza kufuatia tangazo la kuipanua jiji kuu la Addis Ababa.a

No comments:

Post a Comment