Sunday, February 21, 2016

Wakazi Ilemela wamshitaki Dc kwa Waziri...........

SUNDAY, FEBRUARY 21, 2016

Wakazi Ilemela wamshitaki Dc kwa Waziri




Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Manju Msambia.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Manju Msambia. 
By Aidan Mhando, Mwananchi amhando@mwananchi.co.tz
Mwanza. Wakazi wa Kijiji cha Monze, Manispaa ya Ilemela, Mwanza wamemshutumu Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Manju Msambia kutoa kibali cha kufungwa kwa barabara ya Uwanja wa Ndege, Igombe bila kuwashirikisha.
Msambia alikiri kuandika barua kufunga barabara hiyo, akisema ni maagizo ya Serikali.
Wananchi hao walisema hayo juzi mbele ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela.
Mkazi wa kijiji hicho, Tito Kihomole alisema wameachwa kisiwani kama siyo wananchi wa Tanzania, kwani barabara hiyo ina umuhimu kwao na kwamba kufungwa ni kuwakandamiza.
Mkazi mwingine, Grace Leopodi alisema hata wanafunzi wanachelewa kufika shule kwa wakati kutokana na adha hiyo.
Diwani wa Kata ya Shibula, Dede Swira alisema kufungwa kwa barabara hiyo kutarudisha matatizo kwa wananchi hasa wajawazito ambao wanatembea umbali mrefu kufika kwenye kituo cha afya.

No comments:

Post a Comment