Wednesday, February 24, 2016

TPA KUTEKELEZA MRADI MKUBWA WA MIFUMO YA ULINZI NA USALAMA KWA NJIA YA KIELEKRTONIKI

TPA KUTEKELEZA MRADI MKUBWA WA MIFUMO YA ULINZI NA USALAMA KWA NJIA YA KIELEKRTONIKI

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inatekeleza mradi mkubwa wa mifumo ya Ulinzi na Usalama kwa njia ya kielekrtoniki ili kudhibiti usalama wa bandari zake majini na nchi kavu kimtandao.

Mradi huu wa kielektroniki unajulikana kama Intergrated Security System (ISS) unakusanya mifumo mbalimbali ya ulinzi na unafadhiliwa na TPA kwa gharama ya shs. bilioni 9.800.
Mradi huu mkubwa wa ulinzi unahusu ufungaji wa CCTV cameras, ujenzi wa chumba cha kuongozea mitambo yote ya ISS, ufungaji wa taa na minara yake pembezoni mwa ukuta wa bandari, ufungaji wa nyaya mbalimbali, ufungaji wa ‘License Plate Number’ ambapo sasa magari yote yanayoingia bandarini yatakuwa yanasomwa na kurekodiwa namba zake za usajili, ujenzi wa gate house kwenye mageti, ufungaji wa radiation detectors na ‘access control system’.
Jumla ya CCTV cameras 486 zitafungwa ambapo mpaka sasa jumla ya camera 246 zimeshafungwa na kuanza kutumika na camera 144 zilizobaki ufungaji wake unategemewa kukamilika mwezi Machi mwaka huu wa 2016.
Kamera hizi zitasaidia kuiona bandari yote ya Dar es Salaam mpaka kwenye boya la mafuta la SPM Mjimwema, kutokea kwenye chumba kimoja ambacho kamera hizo zinafungwa na hivyo kuwezesha kunasa tukio lolote la uhalifu ambalo linatokea katika eneo husika.
Mradi pia unahusu uboreshaji wa milango ya kuingia ndani ya bandari ambapo mageti maalum ya kisasa yanaendelea kufungwa ili kudhibiti uingiaji ndani ya eneo hili nyeti. Katika mageti haya waingiaji watakaoweza kuingia ni wale tu wenye vibali au vitambulisho maalum ambavyo mitambo  itaweza kuvitambua kielektroniki vitambulisho hivyo ikiwemo wafanyakazi na watumiaji wa bandari.
Mitambo itakayofungwa katika mageti haya itakuwa na uwezo wa kusoma namba za magari yote yanayoingia bandarini na kumbukumbu zake kubaki katika kumbukumbu za Mamlaka.
Ufungaji wa taa na minara yake pembezoni mwa ukuta wa bandari nguzo zimeshasimikwa na taa zinaendelea kufungwa.
Kukamilika kwa mradi huu kutaboresha kwa kiasi kikubwa usalama wa bandari, mali za Mamlaka na mizigo ya wateja na hivyo kuwaongezea imani watumiaji wa bandari kwamba mali zao ni salama katika bandari za Tanzania.

No comments:

Post a Comment