Sunday, July 12, 2015

Bella, Alikiba washidana.

Bella, Alikiba ‘watunishiana’ misuli
Christian Bella anasifika kwa kuwa na tungo makini na sauti
nzuri yenye matamshi mwanana ilhali
ADVERTISEMENT
Dar es Salaam. Christian Bella anasifika kwa
kuwa na tungo makini na sauti nzuri yenye
matamshi mwanana ilhali Alikiba ni maarufu
kwa tungo na sauti inayowavutia wengi.
Itakuwaje wawili hawa wakikutana pamoja?
Jibu la swali hili linajibiwa na Christian Bella,
anayeweka wazi kwamba tayari wamepika
wimbo wa pamoja, wanaotarajia kuuachia mara
baada ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa
Ramadhani.
Mwimbaji huyo wa “Nani Kama Mama” alisema
licha ya kutunga nyimbo nyingi zinazopendwa,
ameamua kutunga wimbo maalum na kuimba
na msanii huyo ili kutoa ladha ya muziki wa
dansi wa kisasa kwa mashabiki wake
wanaomwamini.
“Nimeshajijengea mashabiki kote Afrika
Mashariki hata nje. Video ya “Nashindwa”
imenitambulisha vizuri hivyo, nahakikisha kila
nitakachokipika kwa mara nyingine, kiwe zaidi
ya kile kilichotoka awali,” alisema Bella.
Alisema baada ya Ramadhani anatarajia kuachia
kolabo yake mpya “Namgharimia”,
aliyomshirikisha Alikiba.
“Kolabo hii imefanyika katika studio za Chedaz
Records,” alisema Christian Bella akionyesha
‘umwamba’ mwingine wa tungo za mapenzi
kwa kuachia simulizi tamu ya namna
anavyomgharamia mpenzi wake.

No comments:

Post a Comment