Wednesday, July 15, 2015

Diamond kayajibu haya akiwa Kenya >>> Zari kujifungua, yeye na Siasa.. Mapenzi yake na Zari, MTV, Collabo na Ludacris..

Diamond kayajibu haya akiwa Kenya >>> Zari kujifungua, yeye na Siasa.. Mapenzi yake na Zari, MTV, Collabo na Ludacris..


Diamond
Moja ya Watangazaji wenye majina makubwa East Africa ni Mtangazaji kutoka Citizen TV na Radio, Nairobi Kenya.. Anaitwa Mzazi Willy Tuva, nimekutana na post zake nyingi siku ya leo July 15 2015 kwenye ukurasa wake wa @Instagram, alipata nafasi ya kufanya Exclusive Interview na Diamond Platnumz, majibu yake kwenye maswali kadhaa yako hapa mtu wangu.
Diamond
Hili ni jibu kuhusu Zari kujifungua >>>Zari ( @zarithebosslady ) Kujifungua in The Next 3 Weeks@diamondplatnumz >>>> @msetoea
Hapa kuna majibu pia kuhusu jina la mtoto wake na mpenzi wake Zari the Bosslady >>>> Mtoto Wangu Atazaliwa Tanzania, Jina lake Bado Tunajadiliana na Mamake, Mimi nasema aitwe KENDI mamake anasema aitwe ZARA@diamondplatnumz >>>> @msetoea
Kajibu pia kilichomfanya ampende zaidi Zari >>>> Mwanamke ambae amekubali kunizalia nampa heshima sana, Nimekutana na Wanawake lakini wengi waliniambia ngoja ngoja kama vile nilivyoimba kwa wimbo wangu Nikifa Kesho’ ukizingatia ni Mwanamke maarufu, kiukweli Zari kunizalia imenifanya nimpende Sana‘ >>>> @diamondplatnumz.#MamboMsetoLiveUpdates
Collabo na Ludacris? >>>>NANA ambayo nilifanya na MR FLAVOUR ilikuwa nifanye na msanii wa Marekani LUDACRIS‘ >>>> @diamondplatnumz#MamboMsetoLiveUpdates‘ 
DIA
Kusitisha collabo za nje ya TZ >>>> I was Misquoted, Sijasitisha Kufanya Collabo na Wasanii wa Nigeria ila tu Tumepunguza maana sasa hivi nafanya kazi na wasanii wa pande zote za Afrika, Juzi nimefanya na Donald wa Afrika Kusini na pia nyingine nimefanya na Msanii wa Congo‘ >>>> @diamondplatnumz #MamboMsetoLiveUpdates
Collabo na wasanii wa Kenya je? >>>> ‘Kuhusu Kufanya Collabo na @bahatikenya na @willypaulmsafi@diamondplatnumz Amesema kuimba Gospel itakua tatizo maana ni muislamu labda wimbo ikawa ni neutral maana hataki kuonekana kama anachokoza dini ila anawakubali sana >>>> #MamboMsetoLiveUpdates
Kuna collabo na Wakenya inakuja? >>>> ‘Muda si mrefu Tutafanya kazi na @jaguarkenya , na @collinsmajale . Namkubali @chikuzee_kenya pia ilikuwa nifanye kazi naye lakini aliyekuwa anamdhamini alipotea….lakini hivi karibuni inshallah Tutafanya kazi moja kubwa na msanii wa Kenya ambaye itatusua Afrika Nzima‘ >>>> @diamondplatnumz >>>> @msetoea
mondii
Anaitamani Siasa? >>>> ‘In future Ningependa kuja kuwa Waziri wa Michezo hata nishaambia Mamangu Sana ila si kwa sasa hivi‘ >>>> @diamondplatnumz#MamboMsetoLiveUpdates
Ana matumaini na Tuzo za MTV MAMA >>>> ‘Ukiangalia ile hashtag ya MTV MAMA kwa Mitandao East African Tuko mbele. Sijui ila Tunaweza tukachukua tuzo zote maana, wasipo tupa tuzo yeyote itabidi niwaulize wanaangalia vigezo gani ikija kwenye maswala ya kupeana Tuzo‘ >>>> @diamondplatnumz #MamboMsetoLiveUpdates
diamonte
Kafungukia tena kuhusu kilichofungua milango ya mafanikio yake >>>> ‘Siri ya mafanikio, uvumilivu, Discipline, na Kumwomba Mwenyezi Mungu, Hauwezi kufanikiwa bila kutokea Vikwazo‘ >>>> @diamondplatnumz#MamboMsetoLiveUpdates

No comments:

Post a Comment