Monday, July 13, 2015

Uchakavu wa majengo ya shule tishio kwa wanafunzi.

UCHAKAVU WA MAJENGO YA SHULE
TISHIO KWA WANAFUNZI
Jengo la shule ya msingi Donyonaado.
Na Woinde Shizza,Monduli
Wakati shule nyingi nchini zinafunguliwa baada
kumalizika kwa likizo
Wanakijiji wa kijiji cha Donyonaado kilichopo
wilaya ya Monduli mkoani
Arusha wameeleza wasi wasi juu ya uchakavu wa
jengo la shule ya Msingi
Idonyonaado huenda linaweza kuanguka na
kusababisha maafa kwa
wanafunzi.
Shule hiyo iliyoko umbali wa kilomita 64 kutoka
Monduli mjini
iliyojengwa kwa udongo na mawe na wanakijiji
waliojitoa haina milango
na madirisha hivyo wanafunzi kupata adha ya
vumbi na baridi kali hasa
kipindi cha mvua.
Wanakijiji hao wamesema kuwa hali mbaya ya
miundombinu ya shule hiyo
imewafanya wazazi wengi kusita kuwapeleka
watoto mashuleni hivyo
ameiomba serikali na mashirika binafsi yajitokeze
kusaidia kutatua
changamoto hizo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Donyonaado ,Malulu
Kutetei amesema kuwa licha
ya changamoto za shule hiyo bado wanakabiliwa
na tatizo la ukosefu wa
nyumba bora za walimu pamoja na uhaba wa maji
jambo linalokwamisha
maendeleo ya taaluma shuni hapo.
Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la
Wafugaji la Monduli
Pastodalist Development Initiative (MPDI) ,Erasto
Sanare ameeleza
kusikitishwa na changamoto zinazoikabili shule
hiyo hivyo kushiriki
katika ujenzi wa shule ya kudumu ,ameieomba
serikali isaidia shule
hiyo ambayo ni tegemeo kwa wafugaji.
Licha ya Jamii ya Wafugaji kuamka katika
masuala ya elimu tofauti na
miaka iliyopita bado kuna mazingira duni ya elimu
ikiwemo kukosekana
kwa shule za kutosha,miundombinu mibovu,uhaba
wa maji na vifaa vya
kufundishia na nyumba za walimu

No comments:

Post a Comment