Tuesday, July 14, 2015

Bunge la Rwanda laidhinisha muhula wa 3

Bunge la Rwanda laidhinisha muhula wa 3

  • Saa 6 zilizopita
Bunge la Rwanda limedhinisha awamu ya 3
Wabunge nchini Rwanda wamepitisha mswada utakaoidhinisha kubadilishwa kwa vipengee vya katiba vitakavyoruhusu rais Paul Kagame kuongoza kwa muhula wa tatu.
Katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita mamilioni ya raia nchini Rwanda wamekuwa wakitia sahihi pendekezo la kumtaka rais Kagame kuendelea kuongoza taifa hilo hata baada ya kukamilika kwa muhula wake wa pili.
Kupitishwa kwa mswada huo sasa kunatoa fursa ya kufanyika kwa kura ya maoni ya iwapo ni haki kuruhusu uongozi wa zaidi ya mihula miwili au la.
Rais Kagame mwenyewe amesema kuwa huo utakuwa ni uamuzi wa raia wa nchi hiyo wenyewe.
Mamilioni ya warwanda wametia sahihi ombi la kutaka rais Kagame aendelee kutawala
Wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu wanasema kuwa utawala wa Rwanda unakandamiza uhuru wa kujieleza na hivyo kunyamazisha vyombo vya habari na upinzani.
Iwapo kura hiyo ya maoni itafaulu basi sheria itakuwa imefungua mlango kwa rais Paul Kagame kuwania hatamu ya tatu mwaka wa 2017.
Rais Kagame alichaguliwa kwanza katika mwaka wa 2003.

No comments:

Post a Comment