Tuesday, July 14, 2015

Pichaz na Video ya mapokezi ya Tevez ndani ya Boca Junior.

Michezo

Pichaz na Video ya mapokezi ya Tevez ndani ya Boca Junior unaweza kuzicheki hapa..


Carlos Tevez amerejea katika klabu yake ya zamani ya Boca Juniors iliopo nchini kwao Argentina baada ya kutumia miaka 11 kucheza soka barani Ulaya… Tevez amepokelewa kishujaa na mashabiki na viongozi wa klabu hiyo katika utambulisho rasmi wa kurejea Klabuni hapo.
6
Nyota huyo wa Argentina aliyetumia zaidi ya miaka kumi kucheza soka barani Ulaya katika vilabu mbalimbali ikiwemo Manchester United, Manchester City na Juventus ametambulishwa mbele ya mashabiki katika Uwanja wa Bombonera Stadium ambao unatumiwa na klabu hiyo kama Uwanja wa nyumbani.

Carlos Tevez ameichezea Boca Juniors kuanzia mwaka 2001 hadi 2004 na kutimkia klabu ya Corinthians ya Brazil na baadae akaelekea zake Ulaya. Tevez pia amecheza mechi 72 na timu ya taifa ya Argentina na kuifungia mabao 13, amecheza kombe la dunia mwaka 2006 na 2010 lakini pia amewahi kutwaa medali ya dhahabu ya Olympic mwaka 2004.
Carlos Tevez na Raisi wa klabu ya Boca Juniors Daniel Angelici
Ada ya uhamisho kutoka Juventus kwenda Boca Juniors haijatajwa na Klabu hiyo lakini vyombo vingi vya habari barani Ulaya vinataja kufikia pound milioni 4.6.
Nyota wa soka wa zamani Diego Maradona wa tatu kutoka kushoto akiwa anaangalia utambulisho wa mchezaji huyo.
Nimekuwekea video ya utambulisho wa Tevez hapa mtu wangu.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiun

No comments:

Post a Comment