Monday, July 13, 2015

WAZIRI SAADA MKUYA SALUM AMWAKILISHIA RAIS KIKWETE KWENYE MKUTANO WA UFADHILI WA MAENDELEO ADDIS ABABA

WAZIRI SAADA MKUYA SALUM
AMWAKILISHIA RAIS KIKWETE
KWENYE MKUTANO WA UFADHILI WA
MAENDELEO ADDIS ABABA
Na Mwandishi Maalum, New York
Mkutano wa Mkubwa watatu wa
Kimataifa, unaojadili Ufadhili wa Maendeleo
(FFD3) , umeanza jana jumatatu jijini Adds
Ababa, Ethiopia
Ujumbe Tanzania katika mkutano huu
ambao utakafanyika kwa siku tatu unaongozwa
na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum
akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania , Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mhe. Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum
atauhutubia mkutano huo siku ya jumanne.
Viongozi wengine wa Tanzania
wanaohudhuria na kushiriki mkutano huu
muhimu katika kuchangiza vyanzo vya rasmali za
kusaidia maendeleo na kuwaondoa mamilioni ya
watu kutoka lindi la umaskini hususani kwa
mataifa yanaoyendelea ni pamoja na Waziri wa
fedha kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
Mhe. Omar Yusus Mzee , Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha Bw. Silvanus Likwelile , Mkurugenzi
Mtendaji, Kamisheni ya Mipango, Dr. Philip
Mpango na Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa
Mataifa.
Akifungua Mkutano huo, Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon pamoja na mambo
mengine amesisitiza haja na umuhimu wa uwepo
wa uhakika wa raslimali ambazo si tu zitatumika
katika uboreshaji wa maisha ya watu ambao
wanazidi kuongezea duniani lakini pia kuilinda
sayari duani .
Ban ki Moon amewaeleza washiriki wa
mkutano huo wakiwamo wajumbe kutoka Mataifa
yaliyoendelea na Mashirika ya Kimataifa kuwa
mwaka 2015 unatakiwa kuwa mwaka wa vitendo
na maamuzi.
Akayaainisha mambo muhimu matatu
ambayo yanaufanya mwaka huu wa 2015 kuwa wa
vitendo na kufanya maamuzi. Kuwa kwanza
kufanyika kwa mkutano huo wa Tatu wa Kimataifa
wa Ufadhili wa maendeleo ambao pamoja na
mambo mengine utapokea na kupitisha tamko la
mpango wa ajenda ya utekelezaji wa mpango
mpana juu ya ufadhili wa maendeleo.
Eneo la pili na ambalo ni muhimu kwa
mwaka huu wa 2015 ni mkutano wa kilele wa
kisiasa wa viongozi wakuu wa nchi na serikali
utakaofanyika mwezi Septemba hapa Umoja wa
Mataifa, ambapo viongozi hao wanatarajiwa
kupokea na kupitisha malengo mapya ya
maendeleo endelevu kwa miaka 15 ijayo.
Eneo la tatu na muhimu kwa mwaka huu ni
Mkutano wa Kimataifa kuhusu mabadiliko ya
Tabia nchi ambao utafanyika mwezi Desemba huko
Paris, Ufarasa.
Akizungumza zaidi kuhusu mkutano wa
ufadhili wa maendeleo, Mkuu huyo wa Umoja wa
Mataifa, amesema, ahadi tu za maneno
zinazoishia katika makaratasi hazina tija kwani
kinachotakiwa ni utoaji wa raslimali fedha
pamoja na kuibua vyanzo vipya vya mapato ili
hatimaye utekelezaji wa maeneo hayo matatu
utakuwa ndoto.
Akaongeza kuwa kwa wajumbe kupitisha
ajenda hiyo ya mpango wa utekelezaji kuhusu
ufadhili wa maendeleo ambao pia umeainisha
masuala mengi muhimu yanayohusiana na
utekelezaji wa malengo mapya ya maendeleo
endelevu ni moja ya hatua muhimu sana ya
kuanzisha mwongo mpya wa ushirikiano wa
kimataifa.
Waziri wa   Fedha  Mhe. Saada Mkuya  Salum

No comments:

Post a Comment