Saturday, July 11, 2015

ACT wazalendo kupigwa marufuku na baraza la kilimo tz.

HABARI.BARAZA LA KILIMO
LAPINGA ACT KUTUMIKA KAMA
JINA LA CHAMA Baraza la Kilimo
Tanzania (ACT) limekitaka chama
cha siasa cha ACT – Tanzania
kutotumia jina hilo kwa kuwa tayari
baraza hilo limekwsha sajili jina la
ACT kama kifupi cha jina la Baraza
hilo. Akizungumza leo katika kipindi
cha Hotmix cha EATV kinachoruka
kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 12:00
hadi saa 2:00 jioni, Mwenyekiti wa
Baraza hilo Dkt Sinare Yusuf Sinare
amesema kuwa jina ACT
linatambulika kama kifupi cha
Agricultural Council of Tanzania na
kwa mujibu wa taratibu za hati miliki,
jina hilo (ACT) halitakiwi kutumika na
watu wengine hata kama
litaambatanishwa na maneno
mengine. “Hata kama wakiongeza
maneno, bado kuna ACT, hiyo ni
nembo yetu, tumekwisha andika
barua kwenda kwa msajili wa vyama
vya siasa, pia tumeandika barua
kwenda katika chama hicho lakini
bado hatujapata majibu, nimekwisha
ongea na Zitto Kabwe kuhusu hilo na
kumweleza kuwa wanatakiwa
kurekebisha kabla hatujaenda hatua
za juu zaidi(Mahakamani) ambazo ni
ghali.” Amesema Dkt Sinare.
#HOTMIX
#HABARI BARAZA LA KILIMO
LAPINGA ACT KUTUMIKA KAMA
JINA LA CHAMA Baraza la Kilimo
Tanzania (ACT) limekitaka chama
cha siasa cha ACT – Tanzania
kutotumia jina hilo kwa kuwa tayari baraza hilo limekwsha
sajili jina la ACT kama kifupi cha jina la Baraza hilo.
Akizungumza leo katika kipindi cha Hotmix cha EATV
kinachoruka kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 12:00 hadi saa
2:00 jioni, Mwenyekiti wa Baraza hilo Dkt Sinare Yusuf Sinare
amesema kuwa jina ACT linatambulika kama kifupi cha
Agricultural Council of Tanzania na kwa mujibu wa taratibu
za hati miliki, jina hilo (ACT) halitakiwi kutumika na watu
wengine hata kama litaambatanishwa na maneno mengine.
“Hata kama wakiongeza maneno, bado kuna ACT, hiyo ni
nembo yetu, tumekwisha andika barua kwenda kwa msajili
wa vyama vya siasa, pia tumeandika barua kwenda katika
chama hicho lakini bado hatujapata majibu, nimekwisha
ongea na Zitto Kabwe kuhusu hilo na kumweleza kuwa
wanatakiwa kurekebisha kabla hatujaenda hatua za juu zaidi
(Mahakamani) ambazo ni ghali.” Amesema Dkt Sinare.
#HOTMIX

No comments:

Post a Comment