Friday, July 10, 2015

Urais ccm. Vikao vyafanyika Leo mkutano mkuu kesho.

URAIS CCM: VIKAO VYAFANYIKA LEO,
MKUTANO MKUU KESHO
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
akizungumza na waandishi wa habari nje ya
ukumbi wa NEC,Makao Makuu ya CCM mjini
Dodoma.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi aliwaeleza
waandishi wa habari kuwa vikao vyote vitafanyika
leo kikiwemo cha Kamati ya Usalama na Maadili
pamoja na vikao vya mchujo wa wagombea
kuanzia watano(5) mpaka kupata watatu
(3) ,mgombea wa Urais Zanzibar kisha kesho
tarehe 11 Julai utafanyika mkutano mkuu wa CCM
ambao atapatikana mgombea mmoja wa CCM kwa
nafasi ya Urais.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa za vikao
vitakavyofanyika leo mjini Dodoma kutoka kwa
msemaji wa Chama Cha Mapinduzi, Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye nje ya ukumbi wa
NEC mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment