Saturday, July 11, 2015

MWANAMKE ALIYEJIBADILI JINSIA YAKE YA KIUME HUKO KENYA ASHINDA KESI

Mwanamke aliyebadili jinsia yake ya kiume
na kuwa mwanamke na kutaka jina lake
kubadilishwa kwenye cheti chake cha mtihani
ameshinda kesi yake dhidi ya baraza la
kitaifa la mitihani nchini Kenya.
Mahakama imelazimisha baraza hilo kumpa
Adrey Mbugua cheti kipya kinachoonyesha
hali yake mpya ya kijinsia hasa kwa kuwa
anapokea matibabu ya kufanikisha jinsia
yake kubadilika kabisa.Bi Mbugua alilishitaki
baraza la kitaifa la mitihani nchini humo kwa
kukataa kubadililisha utambulisho wa jinsia
yake kwenye cheti hicho kutoka kwa
Mwanamme na kumtambua kama mwanamke
licha ya amri iliyotolewa katika gazeti rasmi
la serikali.
Jaji Weldon Korir amelipatia baraza hilo hadi siku
45 kubadilisha jina la Adrey katika cheti hicho
kutoka kwa 'Andrew Mbugua' na utambulisho wa
mwanamume na kulibadilisha kuwa jina la kike la
'Audrey Mbugua' bila ya kuweka jinsia yoyote.
Jaji alisema kuwa jinsia ya Adrey kwenye cheti
hicho haiongezi thamani yoyote kwa matokeo yake
wala alama alizopata Audrey na kuondolewa kwake
vile vile hakuna athari yoyote. SOMA ZAIDI>>

No comments:

Post a Comment