Thursday, July 9, 2015

Vito kilwa kumaliza mechi Leo

Timu ya Vito Kilwa ya Kilwa mkoani
Lindi, imemaliza mechi za hatua ya
makundi ya michuano ya Kombe la
Helsinki Cup 2015 kwa kishindo, baada
ya kushinda mechi nne
TIMU ya soka ya vijana chini ya
miaka 11 ya FC Vito Kilwa ya
Kilwa mkoani Lindi, imemaliza
mechi za hatua ya makundi ya
michuano ya Kombe la Helsinki
Cup 2015 kwa kishindo, baada ya
kushinda mechi nne na kutoka
sare moja, hivyo kumaliza ikiwa
kinara wa Kundi BJ/11 ikiwa na
pointi 13.
Zaidi ya timu 1,200 zinashiriki
michuano hiyo ya nne kwa
ukubwa miongoni mwa michuano
ya vijana barani Ulaya,
inayoendelea kushika kasi jijini
Helsinki nchini Finland, ambako
Tanzania inawakilishwa na FC Vito
Kilwa inayomilikiwa kwa ubia kati
ya Sports Development Aid (SDA)
ya Lindi na Liike Finland ya
Finland.

No comments:

Post a Comment