Wednesday, July 8, 2015

Mchezali Mwenye thamani zaidi Ulaya

Sterling:Mchezaji anayethaminiwa zaidi Ulaya 7 Julai 2015 Mshirikishe mwenzako Sterling ndiye mchezaji chipukizi anayethaminiwa zaidi barani Ulaya Nyota wa Liverpool Raheem Sterling ndiye mchezaji chipukizi anayethaminiwa zaidi barani Ulaya kwa mujibu wa utafiti. Raia huyo wa Uingereza ambaye harakati za kuhamia Manchester City, zilitumbukia nyong'o amekadiriwa kuwa mwenye thamani ya pauni milioni 35 na kampuni ya utafiti ya Soccerex inayochapisha Orodha ya wachezaji wenye thamani ya juu ama 20 Football Value Index. Manchester City ilikuwa imeweka dau la pauni milioni £40 lakini ombi lao likakataliwa na Liverpool. Mlinzi wa Manchester United, Luke Shaw ameorodheshwa katika nafasi ya 9, John Stones wa Everton ameorodheshwa wa 16 huku kiungo wa Arsenal Calum Chambers akiorodheshwa katika nafasi ya 19. Kampuni hiyo ya Soccerex imefanya utafiti huo miongoni mwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 wanaocheza katika ligi za bara ulaya. Inatumia vipengee kama umri,nafasi wanayocheza uwanjani,Klabu,urefu wa Kandarasi,mechi walizochezea timu zao za taifa,mechi walizocheza,mabao waliofunga,majeraha na ubora wao kitalanta. ''tukiangalia kwa kina vipengee hivi vyote tunaweza kutathmini uwezo na thamani ya mchezaji.'' ''Hivyo vyote ndivyo vilitusaidia kubaini kuwa Sterling ndiye mchezaji bora na mwenye thamani ya juu zaidi barani ulaya kwa sasa.'' alisema bwana Esteve Calzada Mlinzi wa Paris St-Germain Marquinhos ameorodheshwa katika nafasi ya pili na thamani ya pauni milioni £27.8. Mlinzi wa Paris St-Germain ya Ufaransa ambaye ni raia wa Brazil Marquinhos ameorodheshwa katika nafasi ya pili na thamani ya pauni milioni £27.8. Mchezaji mpya wa Manchester United vilevile ye Uingereza Memphis Depay aliyegharimu kitita cha pauni milioni £31 ameorodheshwa katika nafasi ya tatu akiwa na thamani ya pauni milioni £23.8. Calzada anasema kuwa sheria iliyowekwa na shirikisho la soka la Uingereza ambayo inazilazimisha vilabu vya Uingereza kuwa na takriban wachezaji 8 raia wa Uingereza imeongeza maradufu thamani ya wachezaji waingereza. Wachezaji 4 katika orodha hiyo ni raia wa Uingereza huku9 kati ya 20 bora wakitarajiwa kucheza katika ligi kuu ya Uingereza msimu uja

No comments:

Post a Comment