Saturday, July 11, 2015

Banza atoka hospitali

MUNGU MKUBWA, BANZA ATOKA
HOSPITALI
by Global Publishers Ltd
16 minutes ago
Gladness mallya
BAADA ya mwanamuziki wa Dansi nchini, Ramadhan
Masanja ‘ Banza Stone ’ kulazwa katika Hospitali ya
Mwananyamala , Dar kwa siku saba , hatimaye
ameruhusiwa kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu.
Mwanamuziki wa Dansi nchini, Ramadhan Masanja
‘Banza Stone.
Banza aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo , Jumatano
iliyopita ambapo kwa mujibu wa kaka yake ana nafuu
japokuwa bado hali si shwari kwani daktari aliyekuwa
anamtibu aliwaeleza kwamba ndugu yao huyo ana tatizo
la upungufu wa damu.
“Tunamshukuru Mungu mgonjwa wetu ameruhusiwa
japo bado hali yake haijatengamaa kwani tofauti na
matatizo ya awali ya fangasi za kichwani , anakabiliwa na
upungufu wa damu hivyo tumeshauriwa tumpe vyakula
vya kuongeza damu, ” alisema Hamis .

No comments:

Post a Comment