Friday, July 10, 2015

Diamod na Dewji kusherehesha singida.

MOHAMMED DEWJI AWAAGA RASMI
WAKAZI WA SINGIDA MJINI
Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akiwapungia
wapiga kura wake kama ishara ya kuwaaga rasmi baada ya
kutangaza kutogombea tena ubunge wa jimboni humo wakati
wa mkutano mkubwa wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa
ilani ya CCM kwa miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa
Singida.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog ).
Na Modewjiblog team, Singida
MBUNGE wa Singida mjini na mfanyabiashara maarufu
nchini, Mohammed Dewji amesema hatagombea ubunge wa
jimbo hilo tena baada ya kulitumikia kwa miaka 10 na
kuwezesha maendeleo makubwa katika sekta ya elimu na
afya.
Mbunge huyo alisema hayo akihutubia maelfu ya wananchi
waliokusanyika katika uwanja wa People's Club (MB) wakati
wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya
mwaka 2005/ 2010 na 2010/ 2015 kwenye mkutano mkuu
wa jimbo.Katika utekelezaji huo ametumia shilingi bilioni 5.
Miradi hiyo ni pamoja na kusaidia kuongeza shule za
sekondari kutoka mbili hadi 15, kuwapo kwa vituo vya afya
na kupeleka shule watu wenye mazingira magumu elfu 15.
Alisema ametekeleza majukumu yake ya kusukuma
maendeleo katika jimbo lake la uchaguzi kwa ushirikiano
mkubwa na kufanikisha vipaumbele vya wakati huo ikiwamo
elimu na Afya
Alisema kwamba kujiondoa kwake katika siasa za jimboni
kunatokana na majukumu ya biashara zake kuwa makubwa
pamoja na kutaka kuwa karibu na familia yake baada ya
miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa Singida.
"Ukichukulia kuongezeka kwa-mvi kichwani, ukilinganisha
wakati wa awamo ya kwanza, nafikiri ni busara sasa
kutimiza majukumu haya ya familia ambayo niliyabania
nafasi yake kwa kipindi cha miaka 10.
"Pia siyo siri kwamba majukumu ya biashara zangu
yamebadilika katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. ukuaji
wa biashara zangu umeambatana na kuongezeka kwa
majukumu, hususan mahitaji ya muda zaidi.
Mtazamo huu wa kuipa biashara muda zaidi ni muhimu sana
kwa sababu mafanikio yangu kwenye biashara ndiyo
yaliyoni-wezesha kuwatumikia, na yatakayo-niwezesha
kuendelea kuwatumikia wananchi wa Singida kwa vitendo."
alisema.
Akizungumzia sekta ya afya alisema wananchi wa Singida
walifanikiwa kukabiliana vilivyo na ugonjwa hatari wa Malaria
kwa kugawa vyandarua zaidi ya vyandarua 6000 kwa mama
wajawazito na watoto chini ya miaka 5.
"Kwa kusambaza vyandarua hivi, tulifanyikiwa kupunguza
vifo vya watoto chini ya miaka 5 kwa asilimia hamsini"
alisema akishangiliwa.
Aidha alishirikiana na mamlaka husika kupambana na
ugonjwa sugu wa mtoto wa jicho kwa kupeleka madaktari
bingwa na kufanya kambi kwenye hospital ya mkoa, waliotoa
huduma ya upasuaji wa jicho na kutoa miwani kwa zaidi ya
wananchi 1,000.
"Tulifanikiwa kujenga wodi ya macho, ndani ya hospitali yetu
ya mkoa. Tulifanikiwa kuchangia ujenzi, wa zahanati za
Mungumaji, na Manga ambazo zimekamilika! na zahanati ya
kijiji cha Ititi ambao bado ujenzi unaendelea." alisema
Pamoja na ujenzi huo pia alielezea mafanikio ya kusaidia
baiskeli kwa walemavu na kufunga solar panel, pamoja na
majokofu ya kutunzia dawa, kwenye zahanati za Manga na
Unyambwa!
Akifafanua zaidi katika sekta ya elimu alisema kwamba
walijenga vyumba vya madarasa, kuweka matangi ya maji ya
kuvunia maji ya mvua, vyoo, na kusambaza madawati katika
shule mbali mbali za msingi na sekondari jimboni Singida
mjini.
Aidha alichangia vitabu zaidi 1000, vya masomo ya sayansi
na sanaa, kwa shule zetu zote, za serikali ndani ya
manispaa, ya Singida na tulifanikiwa, kuwapeleka wanafunzi
wa shule ya msingi Ukombozi kwenye ziara ya kujifunza
bungeni.
Akizungumzia sekta ya maji walifanikiwa kuchimba visima
viwili kwenye mtandao wa Suwasa na vingine 45 ndani ya
baadhi ya vitongoji vyetu vya manispaa ya Singida.
Aidha alisema alifanikiwa kusukuma mradi wa visima 10,
unaofadhiliwa na benki ya dunia, akisisitiza kuwa wakati
akiingia mwaka 2005 upatikanaji wa maji safi na salama
ulikua asilimia 23 na sasa upatikanaji wa maji umefikia
asilimia 81.
Pia alisema amefanikiwa kuisukuma serikali, kujenga
barabara za kiwango, cha changarawe ndani ya manispaa na
kufanya manispaa kuwe na barabara zinazopitika kwa kipindi
chote!
Mkazi wa Singida mjini akimwomba Mbunge wake asiache
ngazi kwa maana bado wanamuhitaji baada ya kutangaza
kutogombea tena.
Akiwashukuru wananchi wa Singida alisema kwamba:
"kuwatumikia ninyi imekuwa ni tunu kubwa sana niliyo-
barikiwa katika kipindi hiki cha miaka 10, na najisikia kuwa
nimependelewa kwa kujifunza mambo mengi yanayohusu
Singida na uongozi bora, na hususan mapungufu yake,
ikiwemo mimi mwenyewe."
Alisema dhamira yake kwa wananchi haitokani na nafasi
yangu kama mbunge ama mwanasiasa, akisisitiza kuwa
dhamira yake ya uzaliwa inayotokana na mapenzi aliyonayo
kwao na imani aliyonayo juu ya uwezo wa kuijenga Singida.
"Mapenzi yangu na imani yangu kwenu hayapimiki, na
ninapenda kuwahakikishia leo kuwa, haya yatajitokeza katika
njia nyingine nyingi tu."
Alisema pamoja na kutokugombea katika muhula wa tatu,
lengo lake kuu la kutumikia wananchi wa Singida linabaki
pale pale.
"Naomba nitoe ahadi kwenu! nitaendelea kushirikiana, na
kada wa CCM, mtakaomchagua, kwenye nafasi hii ya ubunge
katika shughuli zote za maendeleo ya jimbo letu! kwani
dhamira yangu, ya kushirikiana nanyi, kujiletea maendeleo,
haikuwa lazima mimi niwe mbunge, bali ilitokana na mapenzi
yangu, kwa Singida na watu wake! "
Mwanamama huyu akiwa haamini macho yake huku machozi
yakimlenga lenga baada ya kusikia Mbunge wake kutogombea
tena ubunge wa jimbo la Singida mjini.
Watoto hawa machozi yakiwalenga na kuonyesha huzuni baada
ya kumsikia mbunge wao akitangaza kuachia ngazi jimbo la
ubunge wa Singida mjini.
Wananchi wa Singida wakisikiliza hotuba ya mbunge wao.
Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akisalimiana
na mkazi wa kijiji cha Kinyampembe kata ya Meria ambaye ni
mlemavu wa macho na miguu aliyefahamika kwa jina moja tu
la Kangariga wakati wa hafla ya mkutano wa kuwasilisha
taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka ya ubunge
wake, ambapo aliitumia nafasi hiyo kutangaza rasmi
kutogombea tena jimbo la Singida mjini jana katika viwanja vya
People's Club.
Mwanamuziki wa kimataifa nchini, Diamond Platnumz akiingia
jukwaani na dancers wake kuwapa burudani wananchi wa
Singida mjini.
Mwanamuziki wa kimataifa nchini, Diamond Platnumz
akitumbuiza wananchi wa Singida mjini wakati wa mkutano
mkubwa wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya
mwaka 2005/ 2010 na 2010/ 2015 kwenye mkutano mkuu wa
jimbo hilo.
Pichani juu na chini ni Diamond Platnumz na ma-dancers wake
wakishambulia jukwaa.
Umati wa wananchi wa Singida ukiwa uchizika na burudani ya
Diamond Platnumz.
Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote na dancers wake
wakitia mbwembwe kwenye show ya kukata na shoka katika
viwanja vya People's Club, Singida mjini.
Chibu Dangote akishambulia jukwaa na dancers wake.
Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote katika hisia kali
kuwapa raha maelfu ya wananchi wa Singida mjini.
Umati wa maelfu ya wananchi wa Singida mjini uliokusanyika
katika viwanja vya People's Club kusikiliza taarifa ya
utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya ubunge wa Mh.
Mohammed Dewji.
Vijana wakimshangilia Chibu Dangote.
Kijana wa Singida mjini (mwenye vest) akiimba jukwaa moja na
Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote.
Ngolololo...cha ngololo now, show me how the do
ngololo...Chibu Dangote akionyesha madoido yake kwa
wananchi wa Singida mjini.
Shangwe za wananchi wa Singida mjini.
Chibu Dangote akiwapa mikono wakazi wa Singida mjini wakati
akiwaaga mara baada ya kutumbuiza.
Kijisehemu cha maelfu ya wakazi wa Singida mjini
waliojitokeza katika mkutano uliotishwa na Mbunge wao Mh.
Mohammed Dewji ambaye amewaaga rasmi.
Kwenye moja na mbili alihusika DJ, Rommy Jones (kulia)
akishow love na mmoja wa ma-dancers wa Diamond, Moses
Iyobo .
Videographer wa MO kutoka Sofia Production, Yusuf Kissoky
akichukua matukio muhimu ya kumbukumbu.
Msafara wa Mh. Mohammed Dewji na Diamond Platnumz a.k.a
Chibu Dangote ukiondoka katika viwanja vya People's Club.

No comments:

Post a Comment