Friday, July 10, 2015

Chadema kutimu wengine Jana.

Waliotuhumiwa Mamluki Chadema
Wavuliwa Uongozi.
Na Bryceson Mathias, Kilosa.
NGUVU ya Umma ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Kata ya Ruaha, Jimbo la
Mikumi, Wilaya ya Kilosa, Morogoro, wamewavua
Uongozi waliokuwa Viongozi wao na kuweka
Kamati ya Muda (Task Force), kwa madai ya kuwa
Mamluki ndani ya Chama chao.
Waliovuliwa Uongozi na kubaki na Uanachama ni
pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kata, George
Banda, Katibu, Ally Mponda, Katibu Mwenezi,
William Temu, Mweka Hazina, Aurelia Mnunga, na
Mjumbe wa Kamati Tendaji, Mwalimu Myami.
Katika Kikao cha ndani cha Julai 2 (Ukumbi wa
Linas), kilichosimamiwa na Mkurugenzi wa
Uchaguzi na Mafunzo wa Chadema Taifa, Benson
Kigaila; Baada ya kusikiliza ‘Tuhuma’ za Viongozi
hao, aliwauliza wanachama wanataka nini, ambapo
wote walipaza Sauti; Wavuliwe Uongozi na kubaki
Wanachama!.
Aidha Tuhuma zilizoelekezwa kwa Viongozi hao, ni
Kuwafukuza Viongozi wenzao Watatu wa Chadema,
kwa kutumia Vifungu visivyokuwemo kwenye Katiba
ya Chadema, ilihali wakijua ni kukinyang’anya
Chadema Ushindi wake halali na kukifurahisha
Chama Mapinduzi(CCM).
Nyingine ni Viongozi hao kuhamisha Vikao vya
Chama, ambapo badala ya kufanyia kwenye Ofisi ya
Chadema Kata, kwa Miezi zaidi ya Minne
walihamishia Vikao na Ofisi kwenye Mgahawa wa
mmoja wa Viongozi hao kinyume cha Katiba.
Kiongozi Mpya, Abasi Longa, alikiri kuchaguliwa
Mwenyekiti wa Muda kati ya Viongozi
waliochaguliwa na Wanachama; Hii ikiwa ni mara
tu baada ya kumvua, Banda aliyekuwa Mwenyekiti,
ambapo, Joram Zacharia, alithibitisha kuchukua
UKatibu aliovuliwa, Mponda.
Mbali ya waliovuliwa nyadhifa kutotaka
kuzungumza na Mwandishi hata walipopigiwa simu
za Viganjani kuelezea walivypokea kuvuliwa
Uongozi na kuwa Wananchama; Aliyekuwa Katibu,
Mponda, pekee alikiri kuondolewa, akisema, “Siasa
ni Kijiti, lazima tupokezana”.alisema
Hata hivyo, Longa alikiri kupokea Fomu za Viongozi
watatu waliovuliwa Uongozi na kubaki Wanachama
wa Chadema, Banda, Mponda na Mnunga, ambao
wametia nia ya Udiwani wa Kata hiyo.
Awali Mponda, alimthibitia Mwandishi wa habari,
kuhusu azma yake kutia nia ya kugombea Udiwani
wa Kata hiyo wakiwemo Viongozi wenzake
waliovulia Madaraka, jambo ambalo limeendelea
kuwawatia Shaka Wana Chadema kuwa, huenda
kulikuwa na kitu nyuma ya Pazia

No comments:

Post a Comment