Saturday, July 11, 2015

Wafuasi wa lowassa walia na kamati Kuu.

Wafuasi wa Lowassa walia na uamuzi wa
Kamati Kuu
Details
Published on Sunday, 12 July 2015 00:08
Written by roryamaendeleo, Dodoma
WAFUASIwa
aliyekuwa
akiwania
uteuzi wa
CCM kuwa
mgombea
urais,
Edward
Lowassa,
ambaye
hakupata
nafasi ya
kuwa
miongoni
mwa
wagombea
bora
watano,
wamepaza
sauti zao wakionesha kutoridhishwa kwa jina la
mgombea huyo kuchujwa katika vikao vya uamuzi.
Mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu
usiku wa kuamkia jana, wajumbe watatu wa kikao hicho
walilalamikia maamuzi hayo.
Mbunge wa Songea Mjini na Waziri wa zamani wa
Awamu ya Nne, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa,
walieleza kutoridhika na uamuzi huo.
Dk Nchimbi alisema hawajaridhika na uamuzi huo kwa
kuwa Lowassa aliondolewa katika hatua za awali na
Kamati ya Maadili aliyodai haina mamlaka kwa mujibu
wa Katiba ya CCM, kufanya hivyo.
Alisema Kamati Kuu ndiyo inayopaswa kufanya uteuzi
huo, na kuongeza kuwa Lowassa pia ana sifa ya
kukubalika ndani na nje ya chama, mojawapo ya vigezo
vilivyowekwa na chama hicho.
Aidha, jana asubuhi, mmoja wa wajumbe wa NEC, Dk
Raphael Chegeni alipokuwa akiingia ukumbini, alipaza
sauti akisema CCM ni chama chao na kuwa
wanakwenda kufanya uamuzi mgumu.
“CCM is our party (CCM ni chama chetu)… tunakwenda
kufanya uamuzi mgumu,” alisema Dk Chegeni na
kuongeza kuwa Lowassa anakubalika kwa wana CCM na
wananchi. Ndani ya Ukumbi wa NEC, wakati wajumbe
wakiwapokea viongozi wakuu wa chama hicho saa 5.50
asubuhi kuanza kikao, waliimba kwa sauti wakitaja jina
la Lowassa. “Tuna imani na Lowassa, oya oya oya…
Lowassa kweli…kweli…kweli…kweli kweli kweli Lowassa,”
waliimba takriban nusu ya wajumbe wakati viongozi hao
wakuu wa CCM walipoingia ukumbini akiwamo
Mwenyekiti wao, Rais Jakaya Kikwete.
Mara baada ya kukaa, Rais Kikwete alisema, “Haijapata
kutokea.” Lakini Lowassa mwenyewe aliwaambia
wanahabari jana asubuhi wakati anaingia katika kikao
cha NEC kuwa hajapata taarifa rasmi za kutopitishwa na
CC na akipata ataongea na wanahabari.
Tangu jina la Lowassa lichujwe na Kamati Kuu,
kumekuwa na hisia kali kutoka kwa wafuasi wake
wakitaka arejeshwe katika mchakato, ili apigiwe kura na
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).
Akifungua kikao hicho cha NEC jana, Rais Kikwete
aliwataka wajumbe kuwa watulivu, kupunguza jazba
akisema ukikasirika, jambo unalotaka kulisema halitatoki
vizuri.
Kikao hicho kilichokuwa na wajumbe 325 kati ya 374
kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana, kilikuwa na ajenda tatu ikiwamo ya kufanya
uteuzi wa wagombea urais wa Zanzibar na wa Jamhuri
ya Muungano ya Tanzania.
Ilitarajiwa kufanya uteuzi huo kwa kupitisha majina
matatu kati ya matano yaliyowasilishwa kwao na Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Hao ni mawaziri Bernard Membe (Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa), Dk John Magufuli (Ujenzi), Dk
Asha-Rose Migiro (Katiba na Sheria) na Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
Mwingine ni Balozi wa Umoja wa Afrika katika Marekani,
Amina Salum Ali. Majina matatu yatakayobaki
yalitarajiwa kupigiwa kura jana jioni katika Mkutano
Mkuu wa CCM kupata mgombea wao wa urais katika
Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment