Saturday, July 11, 2015

Zitto Kabwe auanika wazi Ufisadi wa Freeman Mbowe.

Zitto Kabwe auanika Ufisadi wa
Freeman Mbowe... Adai Tundu
Lissu ni kifaranga, hivyo anamtaka
mama kifaranga....Amegusia pia
kifo cha Chacha Wangwe
Akizungumza katika press conference ya CHADEMA
na waandishi wa habari iliyofanyika leo,
Mwanasheria mkuu wa Chadema, Mh.Tundu Lisu
alisema kuwa mkakati wa kuwachafua viongozi ni
wa siku nyingi ambapo Chama kimefanikiwa
kunasa mawasiliano ya Zitto tangu mwaka 2009
alipokuwa akiwasiliana na akina Denis Msack wa
Mwananchi.
Lissu alisema njama hizi ndio zilizopelekea mpaka
mashtaka ya Ugaidi ambapo katika mahojiano yake
ya Star Tv akiwa na akina Mwigulu Nchemba Zitto
hakukanusha, pia aliandika kwenye mitandao kuwa
Chadema imtose Wilfred Lwakatare
Lissu aliongeza kuwa Zitto mpaka sasa ana magari
mawili ya Nimrod Mkono na Mkono mwenyewe
ndiye amewaambia taarifa hizo. Mkono
amewaambia kuwa amempa Zitto hela nyingi sana
na Zitto alishiriki moja kwa moja kumzuia
mgombea wa Chadema katika Jimbo la Nimrod
Mkono .
====Huu ni ujumbe wa Zitto Kabwe kujibu
mapigo ya Tundu Lissu===
**
Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee
Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. Naamini
Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa
Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe
asifanye kampeni Musoma vijijini.
Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya
orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono
alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime
na Freeman akasema kwenye chama ametoa
mkopo na akalipwa.
Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010
Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya
Slaa. Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam
Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni. Lissu
anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima
limeanzishwa na fedha za chama kutoka
Conservative party?
Nimefanya internship yangu kwa Mkono and
Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba.
Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya
kumtoa Waziri Mkuu Pinda.
Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli
wote. Lissu ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi
namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze
aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka
2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke wazi mkataba
kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo
Club Bilicanas.
They must know I am not a push over. Chacha
died, I won't.
Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake
aliyemzalia watoto hawezi kunyooshea mtu kidole
kuhusu maadili.

No comments:

Post a Comment