Saturday, July 11, 2015

Mkwere kupata mtoto wa kike

MKWERE APATA MTOTO WA KIKE
by roryamaendeleo
9 minutes ago
Mtoto wa Komediani maarufu nchini, Hemedi Maliyaga
‘ Mkwere ’ aliyepewa jina la Shamsa Hemedi Maliyaga .
Chande abdallah
MSANII wa komedi anayeuza sura kupitia Kipindi cha
Mizengwe kinachorushwa katika Kituo cha Televisheni
cha ITV , Hemedi Maliyaga ‘ Mkwere ’ amefunguka kuwa
anajivunia kupata mtoto wa kike baada ya mkewe
kujifungua hivi karibuni.
Mke wa Mkwere na watoto wake , Shamsa na Kamira
mwenye hijabu, aliyevaa tisheti ni mtoto wa mpiga
picha wa ITV .
Akipiga stori na mwandishi wetu , Mkwere alisema mtoto
huyo aliyempa jina la Nurat ni wa pili baada ya wa kiume
na kuongeza kuwa amefurahi zaidi kumpata mtoto wa
kike kwani alikuwa akitamani kwa muda mrefu .
“Mwanangu anaitwa Nurat , kweli nimefurahi sana
nilikuwa na hamu sana ya kumpata mtoto wa kike sasa
furaha yangu imezidi baada ya kumuona , ” alisema
Mkwere .
Wanafamilia wa Maliyaga wakimbeba mtoto huyo .
Mkwere akimbeba mwanaye Shamsa .
Mkwere akiwa na familia yake na Mama Mkwe.

No comments:

Post a Comment