Friday, July 10, 2015

Kikao cha ccm Top 5 yaendelea

RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO
CHA KAMATI KUU YA CCM MJINI
DODOMA LEO, TANO BORA YA
WAGOMBEA KUPATIKANA BAADA
YA KIKAO HIKI
Habari Zinazoendana
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM,
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza
Kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC)
kinachoendelea hivi sasa kwenye Ukumbi wa
White House, Makao Makuu ya CCM, Mjini Dodoma. Kikao
hiki kinapitia majina yote 38 ya Watangaza nia ya kugombea
Urais kwa tiketi ya CCM, ambapo majina matano
yatapatikana baada ya kikao hiki.Kushoto ni Makamu
Mwenyekiti wa CCM - Zanzibar, Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu
Mwenyekiti wa CCM - Bara, Mzee Phillip Mangula (kulia)
pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman
Kinana.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, DODOMA.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakiwa
kwenye Kikao cha kupitia Wagombea wanaowania nafasi ya
Urais wa Tanzania kupitia CCM, ambapo majina matano
yatapatikana katika kikao hiki na kupelekwa kwenye Mkutano
wa Halmashauri kuu ya CCM ili kupata majina matatu
yatakayokwenda kupigiwa kura kwenye Mkutano Mkuu.
Baadhi ya Wapigapicha za Habari wakichukua taswira ya
Wazee wa Kamati ya Ushauri wa Chama.Wazee wa Kamati
ya Ushauri ya CCM ikiongozwa na Rais Mstaafu awamu ya
Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu awamu ya tatu,
Mh. Benjamin Mkapa, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM,
Mzee Pius Msekwa, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mh. Aman
Abeid Karume, Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Cleopa Msuya
pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Sali

No comments:

Post a Comment