Thursday, July 9, 2015

Ozil moyo kwa Wengar

WENGER AMFANYIA OZIL KITU ROHO
INAPENDA
Arsene Wenger ameweka wazi
mpango wake wa kumpa Mesut
Ozil fursa ya kudumu kucheza
namba kumi kuanzia msimu ujao
wa ligi kuu nchini Uingereza na
mashindano mengine.
Ozil, ambaye tangu asajiliwe
kutoka Madrid hajaonesha
kiwango kilichotarajiwa na wengi,
atapewa nafasi hiyo ili kurudisha
makali yake kama alivyokuwa
akifanya Madrid.
Nyota huyo wa Ujerumani
amekuwa mara kadhaa
akichezeshwa nafasi tatu tofauti
na Wenger hali ambayo hata yeye
mwenyewe alionekana
kutofurahishwa nayo.

No comments:

Post a Comment