Friday, July 10, 2015

Ofisi mpya ya CCM kufunguliwa Leo na JK Dodoma

JK AZINDUA UKUMBI WA KISASA WA
MIKUTANO WA CCM MJINI DODOMA
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na viongozi mbali mbali wa mkoa wa Dodoma
mara baada ya kuwasili kwenye sherehe za uzinduzi wa
jengo jipya la mikutano la CCM.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiongoza
sherehe fupi za uzinduzi wa jengo jipya la mikutano la CCM
mjini Dodoma
Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya CRJE Ndugu Hu Bo
akihutubia kwenye sherehe za uzinduzi wa Jengo la kisasa
la mikutano la CCM mjini Dodoma.
Viongozi wakifurahia hotuba ya Mkurugenzi wa CRJE
Balozi wa China Nchi Mhe. LU Youqing akizungumza wakazi
wa uzinduzi wa Jengo jipya la Ukumbi wa mikutano la CCM
mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete
akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana wakati wa sherehe fupi za uzinduzi wa jengo la
ukumbi wa kisasa wa mikutano wa CCM mjini Dodoma.
Bendera za CCM zikipepea nje ya ukumbi wa jengo jipya la
kisasa la mikutano Dodoma Convention Center.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa
salaam za kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM Taifa
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuja kutoa hotuba ya ufunguzi
wa Ukumbi mpya wa kisasa wa mikutano wa CCM mjini
Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Kikwete akihutubia
wakati wa sherehe za ufunguzi wa ukumbi wa kisasa wa
mikutano wa CCM mjini Dodoma
Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akibonyeza tufe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa jengo jipya
la ukumbi wa kisasa wa mikutano la CCM mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akipokea ufunguo kutoka kwa Mkurugenzi wa kampunzi ya
ujenzi ya CRJE kutoka China Ndugu Hu Bo kama ishara ya
kukabidhiwa jengo la ukumbi wa kisasa la mkutano la
Dodoma Convention Center.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya
Kikwete, akimkabidhi mfano wa ufunguo wa Ukumbi mpya
wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre,
Katibu Mkuu wa CCM , Abrahman Kinana, baada ya kuzindua
rasmi ukumbi huo leo, mjini Dodoma
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Kikwete akiwa
kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu,Balozi
wa China Nchini Mhe. LU Youqing na Viongozi wa CCM
mkoa wa Dodoma
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete na viongozi
wengine wa ngazi ya juu CCM wakiwa wamekaa kwenye
meza kuu ndani ya ukumbi mpya wa kisasa wa mikutano
mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania akisalimiana na Waziri Mkuu
Mstaafu Mhe. Fredrick Sumaye kwenye ukumbi mpya wa
mikutano wa CCM mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Kikwete(wa nne toka
kushoto),Makamu Mwenyekiti wa CCM(Zanzibar) Dk.Ali
Mohamed Shein (wa tatu kutoka kushoto) wakiwa kwenye
picha ya pamoja baada ya ukaguzi wa jengo.na Balozi Seif
Idd (kushoto) Makamu wa Rais Dk.Mohamed Bilal,Katibu wa
NEC Oganaizesheni Dk.Mohamed Seif Khatib,Balozi wa
China Nchini Mhe. LU Youqing,Mama Salma Kikwete, Mhe.
Anna Abdala na Mzee Pius Msekwa.
(Picha zote na Adam Mzee)
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments:

Post a Comment