Saturday, July 11, 2015

Simba kutaja mashine mpya matano

Mzungu Simba ataja mashine mpya
tano
KOCHA Mzungu wa Simba, Dylan Kerr, amesema amefanya
tathmini ya kina ya kikosi chake na kubaini
Kocha wa Simba, Dyan Kerr akifanya mazoezi wa wachezaji
wake.
ADVERTISEMENT
KOCHA Mzungu wa Simba, Dylan Kerr,
amesema amefanya tathmini ya kina ya kikosi
chake na kubaini kuwa anahitaji nyota watano
wapya kabla ya kuuanza msimu mpya na
amewahakikishia mashabiki wa Simba kwamba
mambo yatakuwa mazuri watulize presha.
Bosi huyo amewaambia mashabiki kwamba
anahitaji kipa mmoja, beki mmoja, kiungo
mmoja na mastraika wawili ili kumpatia wigo
mpana wa kuchagua kikosi cha kwanza.
Kerr alisema kipa wao namba moja kwa sasa,
Ivo Mapunda ni majeruhi na hafahamiki
atarejea uwanjani lini, hivyo ni vizuri timu hiyo
ikasajili kipa mwingine wa kiwango cha juu.
“Nilifanya tathmini ya wachezaji waliopo kwa
kuangalia historia tu na nafasi walizokuwa
wakicheza, sijatazama uwezo wao uwanjani.
Kwa haraka nimebaini kuwa tunahitaji nyota
watano wapya, kipa, beki, kiungo na straika
wawili, nataka kuwa na kikosi bora,” alisema
Kerr.
Kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya
Vietnam, alisema bado hajaanza kufanya
mazoezi ya mbinu kutokana na baadhi ya
wachezaji waliokuwa na timu zao za Taifa
kushindwa kujiunga na klabu mpaka sasa.
Nyota ambao hawajajiunga na timu ni nahodha,
Hassan Isihaka, Mohammed Hussein
‘Tshabalala’, Abdi Banda, Laudit Mavugo na
Jonas Mkude aliyerejea nchini mwishoni mwa
wiki iliyopita akitokea Afrika Kusini
alikokwenda kufanya majaribio ya soka la
kulipwa.
“Hatuwezi kufanya mazoezi ya mbinu wakati
wengine hawajajiunga na sisi, tunafanya
mazoezi ya viungo hapa na ufundi kidogo,
mbinu na namna ya kushinda mechi ni baadae
tukikamilika wote,” alisema Kerr.

No comments:

Post a Comment