Thursday, July 9, 2015

Nacte yafuta usajili wa vyuo vitatu.

NACTE yavifutia usajili vyuo vitatu (3)
na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita
(16)
Dar es Salaam, 24 Juni 2015 — Katika jitihada za kuinua
ubora wa elimu ya ufundi nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya
Ufundi (NACTE) limevifutia usajili vyuo vitatu na kuvishusha
hadhi vyuo kumi na sita.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE Dkt. Adolf B.
Rutayuga alisema kuwa, hatua hiyo imefikiwa baada ya vyuo
husika kushindwa kurekebisha kasoro zilizobainishwa na
NACTE.
“Kwa kutumia Sheria ya Bunge Sura Na. 129 na Kanuni za
Baraza za Usajili (2001) na zile za Ithibati na Utambuzi
(2001), mnamo tarehe 20 Februari 2015, Baraza lilitoa notisi
ya siku 30 kwa taasisi na vyuo vilivyokiuka taratibu na vyenye
mapungufu makubwa ya Usajili na Ithibati kupitia taarifa yake
kwa Umma. Notisi hii ililenga kuzipa taasisi na vyuo nafasi ya
kujitetea na kufanya marekebisho yaliyobainishwa,” alieleza.
Kaimu Katibu Mtendaji huyo ambaye ni Mkurugenzi wa
Ushauri na Malezi ya Taasisi na Vyuo vya Ufundi NACTE
aliwaambia waandishi wa habari kuwa, Baraza linakiri kuwa
taasisi na vyuo vingi vilivyopewa maelekezo ya kufanya
marekebisho vimechukua hatua mbalimbali za kurekebisha
mapungufu yabainishwa. Hata hivyo alisema hadi kufikia leo
tarehe 24 Juni 2015 yaani siku 124 baada ya Notisi ya
Baraza, kuna vyuo ambavyo havijachukua hatua yoyote ya
kurekebisha mapungufu yake.
“Baraza limeamua kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria na
Kanuni zake kwa taasisi na vyuo vyote vilivyoorodheshwa
kwa makosa yafuatayo, moja kumalizika kwa muda wa
Usajili wa Awali (Preparatory Registration) na Usajili wa
Muda (Provisional Registration); pili kutoanza mchakato wa
kupata Ithibati baada ya kupata Usajili Kamili; tatu kumalizika
kwa muda wa Ithibati na kutochukuliwa hatua ya kuomba
upya Ithibati (re-affirmation); na nne taasisi na Vyuo kuamua
vyenyewe kusitisha kutoa mafunzo kwa sababu mbali mbali,”
alifafanua
Vyuo vilivyofutiwa usajili ni pamoja na Dar es Salaam College
of Clinical Medicine cha jijini Dar es Salaam kilichokuwa
kimepatiwa usajili wa awali, Ndatele School of Medical
Laboratory Sciences cha Dar-es-Salaam kilichokuwa
kimepatiwa usajili wa awali na Institute for Information
Technology cha jijini Dar es Salaam pia chenye namba za
usajili REG/EOS/014.
Taassi/vyuo vilivyoshushwa hadhi baada ya kushindwa
kutiza mashart ni pamoja na Sura Technologies – Dar es
Salaam, Institute of Management and Information
Technology – Dar es Salaam, Techno Brain - Dar es Salaam,
Ministry of Agriculture Training Institute Igurusi – Mbeya,
Mbozi School of Nursing – Mbeya, KCMC AMO
Ophthalmology School – Moshi, KCMC AMO Anaesthesia
School – Moshi, Advanced Pediatrics Nursing KCMC –
Moshi.
Vingine ni, AMO Training Centre Tanga – Tanga, CATC –
Songea, CATC – Sumbawanga, COTC Maswa – Shinyanga,
COTC – Musoma, Dental Therapists Training Centre –
Tanga, Ngudu School of Environmental Health Sciences –
Kwimba na KCMC AMO General School – Moshi.
Kuhusu NACTE
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo
kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, kwa lengo
la kusimamia na kuratibu taaluma zinazotolewa na taasisi na
vyuo vva elimu ya ufundi nchini, ambavyo siyo vyuo vikuu au
vyuo vikuu vishiriki. Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza
na kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini kwa kusimamia
kikamilifu shughuli za kuendesha mafunzo ili tuzo
zinazotolewa na taasisi na vyuo ziwe na ubora unaokubalika
kitaifa na kimataifa.

No comments:

Post a Comment